Muziki wa kizazi kipya kanda ya nyanda za juu kusini wawasha Indiketa!!

Sanaa ya muziki wa kizazi kipya kanda ya nyanda za juu kusini imeanza kuwasha endiketa baada ya kuibuka watayarishaji wa muziki na video wanaotoa kazi zenye ubora wa hari ya juu, watayarishaji hao wanapatikana pandeza NJOMBE wilaya iliyopo mkoani IRINGA, ambapo baadhi ya wasanii maarufu na chipukizi tayari wameshafanya kazi katika studio hii inayoitwa SOUND POWER chini yaproducer B jayz
Wasanii hao ni TUNDA MAN na wimbo wake rudi nyumbani (remix),DK KUMPENEKA na wimbo unaoitwa "wanipa vitamu" ambao bado hajauachia, na baadhi ya maunderground wanaokuja juu katika vituo mbalimbali vya redio kwa sasa kama vile 2N, Y D.DOX, YB, ambao pia wamefanya video chini ya studio ya MJS chini ya muongozaji MAJID MSIGWA kama unavyoona pichani kutoka kushoto ni masanii SIR ONE wakundi la WISE CREW ambaye naye anawakilisha nyanda za juu kusini, producer B jayz namuongozaji wa video MAJID MSIGWA kutoka pande pande za NJOMBE.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment