SHINDANO LA JISHINDIE SAFARI YA KITALII TANZANIA LAANZISHWA!!

Waziri wa Maliasili Mh. Shamsa Mwangunga akizindua rasmi shindano la "Jishindie Safari ya Kitalii" litakaloendeshwa na Bodi ya Utalii Nchini TTB wakati wa maonyesho ya 33 ya biashara ya kimatifa yaliyomalizikika hivi karibuni katika viwanja vya mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam Kushoto ni katibu mkuu Wizara ya Maliasili Dk. Ladslaus Komba na kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Peter Mwenguo wakishuhudia uzinduzi huo.
Afisa uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Geofrey Tengeneza akionyesha kipeperushi kinachoelezea na kutangaza shindano hilo ambalo mshindi atajishindia kutembelea mbuga za wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii nchini.


MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA SHINDANO HILI.Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeanzisha shindano lijulikanalo kama “Jishindie Safari ya Kitalii Tanzania” kwenye kampeni yake ya kuhamasisha Utalii wa ndani. Kwa kupitia kauli mbiu isemayo “Utalii Uanze kwa Mtanzania Mwenyewe”. Katika shindalo hili watanzania wote waishio Tanzania wanaruhusiwa kushiriki kwa kujibu maswali kumi na kujishindia safari ya kutembelea moja ya vivutio vya Kitalii vilivyopo Tanzania.
Shiriki shindalo hili kupitia kwenye magazeti ya Kiswahili, au kwenye fomu maalum zinazopatikana kwenye ofisi za Bodi za Dar-es-Salaam na Arusha na kwa kupitia kwenye Tovuti (website) ya Bodi ya Utalii Tanzania “http:/www.tanzaniatouristboard.com” .
SHERIA NA TARATIBU YA KUSHIRIKI KWENYE SHINDANO LA JISHINDIE SAFARI YA KITALI TANZANIA.
A. SHERIA:
1. Shindano hili ni kwa ajili ya watanzania waishio Tanzania tu na litaanza tarehe 4/July/2009, kuisha tarehe 24/Sept/2009 saa kuminambili jioni.
2. Washiriki watakaojibu maswali yote kwa usahihi ndio watakaoingizwa kwenye droo kubwa ya kupata washindi wawili.
3. Washindi wawili watakao patikana wataruhusiwa kumchagua mtu mmoja kila mmoja atakayeambatana wakati wa kwenda kutembelea vivutio vya utalii Tanzania.
4. Wafanyakazi pamoja na familia zao wa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake zote hawataruhusiwa kushiriki kwenye shindano hili.

B. NAMNA YA KUSHIRIKI:
1. Tembelea tovuti (website) ya Bodi ya Utalii Tanzania http:/www.tanzaniatouristboard.com na nenda sehemu iliyoandikwa Jishindie safari ya Kitalii jibu maswali na uyatume tena.
2. Jibu maswali yote kwa kupitia mtandao (online) au kwenye form zinazopatikana katika ofisi za Bodi ya Utalii Dar-es-Salam na Arusha na kwenye magazeti ya Kiswahili.
3. Hakikisha umejaza jina lako kamaili na barua pepe (e-mail) na namba ya simu kwenye nafasi unayotakiwa kujaza.
C. JINSI YA KUMPATA MSHINDI NA ZAWADI:
1. Droo ya kumpata mshindi itachezeshwa tarehe 25/Sept/2009 saa nne asubuhi, Mshindi atatangazwa wakati wa kilele cha siku ya Utalii duniani tarehe 27/Sep/2009 mkoani Iringa na wataarifiwa kwa kupitia kwenye magazeti, simu na barua pepe.
2. Washindi wawili watazawadiwa safari ya wiki moja ya kutembelea baadhi ya vivutio vya Utalii Tanzania, hususan Hifadhi ya taifa na maeneo ya kihistoria na kitamaduni.
3. Bodi ya Utalii Tanzania itagharamia gharama ya Usafiri, Chakula na Malazi kwa washindi na mtu mmoja atakayeambatana naye.

KUPONI YA MASWALI

JINA KAMILI:-------------------------------------------------------- SANDUKU LA POSTA:-------------------------KAZI YAKO/MWANAFUNZI:----------------------------------------- NAMBA YA SIMU:----------------------------- BARUA PEPE (Email- Address): ---------------------------------------------
JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA USAHIHI ILI UJISHINDIE SAFARI YA KWENDA KWENYE VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA
ANDIKA HERUFI YA JIBU SAHIHI KWENYE KISANDUKU
1. Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Barani Afrika. Mlima huu una urefu wa mita ngapi kutoka usawa wa bahari?
a)
Mt 5,895
b) Mt 6,992
c) Mt 5,775
2. Ipi kati ya majibu yafuatayo si Hifadhi za taifa nchini?
a)
Katavi
b) Mikindani
c) Udzungwa
3. Moja kati ya haya majibu si Kivutio cha Kihistoria
a)
Kijiji cha Butiama
b) Vita vya Majimaji
c) Dodoma
4. Eneo lipi kati ya haya siyo kati ya maeneo ya Urithi wa Dunia(World Heritage Sites)
a)
Kilwa Ruins
b) Zanzibar Stone Town
c) Dodoma
5. Bonde la Ngorongoro limetajwa kama Ajabu laNane la Dunia lipo kwenye mkoa wa
a)
Arusha
b) Moshi
c) Mara
6. Michoro ya Mapangoni ya watu wa kale kwenye miamba ya mawe (Rock Painting) inapatiakana
a)
Kolo – Kondoa Irangi
b) Mapango ya Amboni – Tanga
c) Mbozi – Mkoa wa Mbeya
7. Henry Stanley alikutana na Dk. David Livingstone magharibi ya Tanzania kwenye kijiji kiitwacho
a)
Mpanda
b) Ujiji
c) Tabora
8.
Mwaka 1959, Dk. Leakey na Mkewe Dk. Mary walivumbua fuvu la mtu wa kale aitwaye Zinji, sehemu iitwayo
a) Loliondo
b) Olduvai Gorge
c) Engaruka
9.
Tanzania inasifika sana ulimwenguni kwa ukarimu wa watu wake na vivutio vya utalii
A. NDIYO, B. HAPANA
10.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ipo Mkoa wa Mbeya ?
A. NDIYO, B . HAPANA

Kumbuka ukishajaza, tuma Kuponi hii kwenda Ofisi yoyote ya Bodi ya Utalii kama ifuatavyo:
1. Bodi ya Utalii Makao Makuu, S.L.P 2485 DSM , Jengo la IPS Gorofa ya Tatu.
2. Bodi ya Utalii Tawi la Arusha, S.L.P 2348 Arusha, Barabara ya Boma.
3. Kituo cha Habari za kitalii, barabara ya Samora, Jengo la Masalamati DSM.
4. Nukushi/FAX +255 22 2116420Kwa maelezo zaidi Piga simu namba Simu: +255 22 2111244/5 Maswali yanapatikana pia kwenye mtandao wa TTB bofya hapa. http://www.tanzaniatourtistboard.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment