Radio VOA inawaletea mahojiano na Ras Makunja katika kipindi cha "Mziki Kutoka Afrika"!!

Radio Voice of America idhaa ya kiswahili inayorusha matangazo yake kutoka mjini Washington DC, inawaletea mahojiano maalumu na kiongozi wa The Ngoma Africa band,Ebrahim Makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu",majiano hayo yatasikika wakati wowote leo hii jumatano 8-07-2009 kwa wasikilizaji wa Afrika mashariki na kati,Mtangazaji wa radio VOA Bw.Abdushakur anamuhoji Ras Makunja kuhusu nafasi ya mziki wa dansi katika soko la kimataifa?Pia Misukosuko na mitihani gani? iliyokumbana na bendi hiyo hadi kufikia mafaniko ya kuhurudisha mziki wa dansi kwa kasi kubwa katika imaya ya jamii na washabiki wa ulaya ambako mziki huo wa dansi kwa sasa unatamba! mtangazaji wa VOA Bw.Abdushakur ambaye pia bingwa wa maswali alimuhoji mengi Ras Makunja kuhusu mziki na nyimbo za ngoma africa ambazo mara nyingi zimekuwa na ujumbe au ushauri muhimu kwa jamii,pia miziki wa dansi kwa nini ?umeelekeza kasi kubwa ulaya? Hili kusikiliza mahojiano hayo na majibu ya Ras Makunja pia unaweza kusikiliza katika mtandao wa radio VOA http://www.voanews.com/swahili ingia katika mziki kutoka Afrika.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. helo Ras Makunja nakupa big 5,kazi yako nzuri sana ,nakukubali kamanda.

Post a Comment