Kwa wale ambao hawakuweza kushuhudia utoaji wa heshima za mwisho kwa Marehemu Michael Jackson kupitia vyombo mbalimbali vya Luninga ikiwepo TBC1 hivi ndivyo mambo yalivyokuwa kwa ufupi katikaukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles Marekani ambapo zaidi ya watu 80.000 walihudhuria utoaji waheshima za mwisho wakiwemo watu maarufu mablimbali katika picha kama unavyoona, ni ndugu wa Marehemu Michael Jackson wakitoaJeneza la Marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jackson ,mwanamuziki huyo alifariki juni 25 nchini marekani na kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa anatarajiwa kuzikwa leo au kesho mara baada ya mwili wake kuagwa rasmi jana (picha kwa hisani ya mtandao).
Ndugu na jamaa wa Marehemu Michael Jackson wakiwa wamekaa wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Michael Jackson.
Mwanamuziki Steve Wonder akiimba wakati watu zaidi ya 80.000 walipotoa heshima zao za mwisho kwa Gwiji wa muziki wa Pop Duniani Marememu Michael Jackson.
Jannet Jackson Dada wa marehemu Michael Jackson akiwa na watoto wa marehemu kulia Catherine na Paris na ndugu zao wengine.
0 comments:
Post a Comment