WAFANYAKAZI BANDARI YA DAR ES ALAAM WAKIMBIA PEKUPEKU KUEPUKA TISHIO LA MAHARAMIA!!


Leo asubuhi iliripotiwa kuwa Maharamia wameigia katika Bandari ya Dar es alaam na boti moja ambayo haikutambulika katikaRada hivyo kutishia Usalama wa wafanayakazi pamoja na mali zilizopo katika Bandari hiyo kwani habari zilisema Boti hiyo ilikuwa imebeba watu ambao hawakujulikana mwenendo wao na mabobu ambayo yangeweza kulipuka wakati wowote.
Hata hivyo FULLSHANGWE ilipofuatilia habari hizo ilikutana na mwanausalama mmoja wa bandarini hapo ambaye hakupenda kutaja jina lake na alipoulizwa kilichotokea bandarini hapo mpaka wafanyakazi wanakimbia hovyo alisema "Sina habari zozote zaidi ya tangazo lililotolewa na Kikosi Cha Zimamoto bandarini hapo kwamba wafanyakazi wote tuondoke na kutoka nje ya Bandari kwani kulikuwa nahatari",
Kitu kilichowafanya wafanyakazi kutoka mbio na kuelekea nje ili kuokoa maisha yao, hata hivyo FULSHANGWE iliendelea kudodosa habari kamili juu ya tukio hilo na kuongea na baadhi ya wafanyakazi mbalimbali waliokuwa nje ya Bandari hiyo, ambao walisema kwamba walipata taarifa baada ya muda kuwa kumbe lilikuwa ni zoezi la kwaida kwa vikosi vya usalama na ulinzi bandarini hapo ili kujiweka sawa katika kujikinga kwa majanga kama hayo mara yatakapotokea, mpaka sasa jeshi la polisi halijathibitisha kama kweli kulikuwa na maharamia wamevamia Bandarini hapo au lilikuwa ni zoezi la kawaida kama baadhi ya wafanyakazi walivyoelezea, mara tupatapo taarifa kamili kutoka kwa wahusika tutawaletea kadri tutakavyozipata
Hata hivyo wakati tukikaribia kuruka hewani habari zinasema Kamanda wa kanda maalum Afande Suleiman Kova amethibitisha kwamba tukio lililotokea leo asubuhi Bandarini lilikuwa ni zoezi na halikuwa tukio la kweli kwamba maharamia wamevamia hili lilikuwa ni zoezi la kwaida kwa vyombo vyetu vya usalama ili kujiweka sawa kwa ujangili na matukio kama hayo mara yatakapotokea (habari ndo hiyo wadau).

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment