MAREHEMU KIDUME ALIKUWA MTU MAHIRI KATIKA MAJUKUMU YAKE!!

Kwa mujibu wa habari kutoka katika Blogu ya Jiachie inayoendeshwa na mwanafamilia mwezetu katika libeneke la kublog Michuzijunior kuna taarifa za kifo cha lafiki yetu mkubwa aliyefahamika kwa jina la Kidume, tunasikitika kuondokewa na rafiki yetu huyu na tunasema tulimpenda lakini mungu ndiye aliyempenda zaidi marehemu kidume atakumbukwa kwa mchango wake wa kiusalama katika matamasha mbalimbali ambayo wana wa FULLSHANGWE tulikuwa tukihudhuria kwa ajili ya kazi zetu za kuipasha habari jamii, alikuwa mahiri katika jukumu zima la ulinzi na Usalama mara unapomkabidhi majukumu na pia alizingatia taratibu zinazolinda haki na kazi yake ili kutowakwaza mashabiki , inasemekana marehemu Kidume amefia nyumbani kwake jana kwa ugonjwa wa Apendix mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Amin.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment