Naye Bingwa wa dunia wa KIckboxing Japhet Kaseba amesema amejiandaa kuonyesha upinzani kwa mpinzani wake Francis Cheka ukizingatia kuwa ni bondia mzuri, ameongeza kuwa kabla ya kuhamia kwenye mchezo wa Kickboxing alishawahi kucheza mapambano kama nane hivi ya Boxing na akashinda yote hivyo anazielewa vizuri sheria za Boxing na atacheza kwa uwezo wake na mbinu mmbadala ili kumtwanga mpinzani wake Francis Cheka mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo.
Bingwa wa masumbwi wa Dunia katika mkanda wa ICB Francis Cheka akionyesha ngumi yake kama ishara ya kuteketeza mpinzani wake Japhet Kaseba mara baada ya mkutano na waandishi wa habari leo
Japhet Kaseba akizungumza na waandishi wa habari kuelezea uwezo wake katika mchezo wa boxing pamoja na kwamba ni Bingwa wa Kickboxing na ana uwezo mkubwa wa kucheza mchezo huo kushoto ni rais wa shirikisho la ngumi za kulipwa tanzania PST Emanuel Mlundwa.
FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA KUPAMBANA MWEZI UJAO!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment