WAREMBO REDDS MISS ILALA 2009 KUTEMBELEA MBUGA ZA NGORONGORO!!

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Redds Miss Ilala 2009 Jackson Kalikumtima akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo kuelezea mikakati mbalimbali iliyopangwa ili kuhakikisha kanda hiyo inatoa Vodaco Miss Tanzania 2009, shindano la Redds Miss Ilala linatarajiwa kufanyika Agosti 7 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee ji9jini Dar es alaam ambapo kabla ya kufanyika kwa shindano hilo warembo watakuwa na ziara ya kutembelea mbuga za Ngorongoro mkoani arusha kuazia juali 22 mpaka 26 na watakaporudi watashiriki kwenye onyesho la vipaji litakalofanyika Lamada Hotel julai 28
Warembo wanaoshiriki kwenye shindano hilo ni Fatma Bongi, Everline Gamasa, Julieth Lugembe, Magreth Motau, Lilian Nyamizi Mihayo, Irene Karugaba, Neema Doreen Kasunga, Winnfrida Mmari, Husna Ahmed Doris Luis, Groly Mwandani, Pendo Lema, Anne Mkandawile, Khadija Mhecha, Sylivia Shally, Gladness Shao na Zena Mbasha pamoja na mwalimu wao Regina Joseph na matron Nelly Kamwelu aliyekuwa Miss Ilala namba mbili mwaka jana.
Hapa baadhi ya Warembo wakionyesha pozi mbalimbali jinsi ya kupiga picha katika shindano hilo pia atapatikana mshindi wa Miss Photogenic yaani mrembo mwenye mvuto zaidi katika picha.
Washiriki wa shindano la kumsaka mrembo wa Redds Miss Ilala 2009 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment