Mbunifu wa mavazi Asia Idarous akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya Habari maelezo leo wakati alipozungumzia onyesho lao la mavazi linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma Julai 17, onyesho hilo litapambwa na bendi ya Kalunde inayoongozwa na mwanamuziki Deo Mwanambilimbi huku wabunifu kadhaa wakishiriki kuonyesha nguo zao, wabunifu hao ni Asia Idarous mwenyewe, Gymkana na Grace Matovolwa, katika picha kulia kwake ni Mbunifu Gymakana (Paka Wear)
Meneja mkuu wa Bendi ya Kalunde Debora Nyangi akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipoelezea juu ya bendi hiyo kutoa burudani katika onyesho la Usiku wa Kanga Dodoma lilioandaliwa na Asia Idarous Fabak Fashion na Sharon Fashion Dodoma litakalofanyika Julai 17 kwenye ukumbi wa Kilimani.
0 comments:
Post a Comment