AKUDO IMPACT WAMALIZA KAZI MAONYESHO SABASABA!!

Kiongozi wa Akudo Impact Christiane Bella mwenye nguo nyekundu akiongoza wanamuziki wenzie katika kushambulia jukwaa wakati walipofanya onyesho la mwisho kwenye banda la Sereneti katika maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa sabasaba yaliomalizika leo kwenye viwanja vya mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam ambayo yameonyesha kuwa na mafanikio makubwa kwa makampuni yaliyoshiyiki katika kuonyesha bidhaa zao.
Vijana wa masauti Akudo Impactwalishangwesha vilivyo kwenye banda la Serengeti kama unavyowaona wakiwa jukwaani na kuwajibiki vilivyo kwa mashabiki wao wakiati wa maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba yaliyomalizika leo kwenye viwanja vya mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam.
Mzee Magoma Moto ambaye haoni soo kukata viuno na kuwapa raha mashabiki wake wakati awapo kazini kama unavyoona akifanya vitu vyake kwenye banda la Serengeti huku chupa ya kinywaji hicho ikiwa kichwani.
watu mbalimbali wakiwa kwenye banda la Serengeti ili kupata kilaji.
Kilajisaina ya Serengeti Lager, The Kiki na Stela Artois kinachotengenezwa na Kampuni ya Serengeti Breweris Ltd kikiwa kimepangwa tayari kwa kuuzwa katika maonyeshoya sabasaba yaliyomalizika leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment