SASATEL YAMALIZA MAONYESHO KWA MAFANIKIO MAKUBWA!!

Baadhi wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Sasatel wakiwa katika picha ya pamoja kwa furaha mara baada ya kumaliza kazi ngumu iliyowachukua takriban siku tisa katika maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa yaliyomalizika leo kwenye viwanja mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam,
Meneja wa maouzo ya rejareja (Retail Sales Manager) aliyetambuliwa kwa jina moja la Gerrad amesema wameshiriki maonyesho hayo kwa mafanikio makubwa japokuwa bado hawajafanya tathmini ya mauzo hayo lakini dalili zinaonyesha kuwa mafanikio katika mauzo yamekuwa ya hali ya juu sana kwa muda wote wa maonyesho haya tangu yalipoanza mpaka sasa tunapofunga bandaletu watu wametupokea vizuri na nina imani tutapanua sana huduma yetu ukizingatiakwamba ndiyo kwanza kampuni yetu imeanza.
Wafanyakazi wa kampuni ya Simu za mkononi Sasatel wakifanya majumuisho ya mwisho mara baada ya kazi nzima ya maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa yaliyomalizika leo kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa kuanzia kulia ni Patricia Semiti,Emilly Burrows,Zaitun Fadhil na nyuma yao ni Malik Fundikira.
Mruta Khamis ambaye ni Direct Sales Manager wa sasatel akitoa maelekezo kwa mmoja wa wafanayakazi wa kampuni hiyo Patricia Semiti jinsi ya kutoa maelezo kwa wateja wanaotembelea Banda hilo kuhusu simu ya mezani ambayo pia unaweza kuunganishwa na mtandao yaani Internet kwa wakati mmoja wakati wa mo0nyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa yal;iomalizika leo kwenye viwanja vya mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa yaliyomalizika leo jijini Dar es alaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment