VODACOM YATANGAZA MWISHO WA PROGRAMU YA TUZO MILIONEA!!

Meneja Matukio na Promosheni wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa(kushoto)akimpigia simu mshindi wa muda wa maongezi yenye thamani ya shilingi 100,000 Joel Mwakipesile mkazi wa Manzese aliyejishindia katika program ya Tuzo Milionea.(kulia)Mkurugenzi wa michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Milao.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imetangaza mwisho wa program yake ya Tuzo Draw iliofanyika kwa muda wa miezi kumi na mbili.
Programu ya Tuzo Draw ilikuwa na awamu mbili, ya kwanza ilianza mwezi wa nne 2008 na kuisha mwezi wa tatu 2009 iliojulikana kama TUZO DRAW NA TUZO POINTS. Wakati awamu ya pili ya TUZO MILLIONAIRE ilianza mwezi wa nne (Aprilli) mwaka huu na itaisha wiki hii wakati mshindi mmoja atakapojinyakulia jumla ya shilingi Milioni mia moja fedha taslimu.
Katika awamu ya pili ya Tuzo Milionea Vodacom Tanzania imewazawadia jumla ya washindi 59 muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi laki moja moja. Washindi hawa walipatikana katika droo zilizoendeshwa kila siku chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha.
Hadi sasa Vodacom Tanzania imeshatoa zawadi ya zaidi ya biliioni moja fedha taslim kwa wateja wake kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.
“Kwa kuwa tunaelekea mwisho wa programu hii na droo kubwa kuchezeshwa wiki hii tarehe 18.6.09 Live katika kituo cha televisheni cha ITV, napenda kuwaambia wateja wa Vodacom kuwa Tuzo droo imeisha rasmi tarehe 14 saa sita usiku.”
Meneja Matukio na Promosheni Rukia Mtingwa alisema, Vodacom Tanzania mapema mwezi Machi mwaka jana ilianzisha programu ya uaminifu ya tuzo pointi/Droo lengo likiwa ni kuwashukuru wateja wa Vodacom Tanzania kwa kuufanya mtandao wa Vodacom Tanzania kuongoza hapa Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment