The Ngoma Africa band kutingisha tamasha la Masala Festival,Hannover,Ujerumani!!


Bendi ya mziki wa dansi "The Ngoma Africa Band" yenye maskani yake mjini Oldenburg,Ujerumani.wataupeleka mzimu wa dansi katika jukwaa kubwa la maonyesho la Masala Festival,mjini Hannover,Ujerumani siku ya jumapili ya Juni 14 -2009 .
Bendi hiyo yenye tabia ya kuwapeleka mashabiki mchaka mchaka kwa muziki wake murua huko ughaibuni, inatarajiwa kutumbuiza majira ya saa 10.00 alasiri,ambapo washabiki wa nyimbo za kiswahili na muziki wa dansi wanaisubiri kwa hamu bendi hiyo, iliyofanikiwa kujizolea umaarufu kwa kutumia vionjo vya midundo ya dansi ya kibongo.
Kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Ras makunja ataliongoza kundi hilo jukwaani kwa kazi moja tu, nayo ni kuwadatisha na kuwapa shangwe mashabiki! hebu wasikilize hapa mdau upate uhondo wa kazi yao nzuri www.myspace.com/thengomaafrica pia wasiliana nao kwa ngoma4u@googlemail.com pia unaweza kupata habari zaidi bofya hapa
http://www.africa-news.eu/news/entertainment/the-ngoma-africa-band-continues-to-thrill-fans.html

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. te!te! wanamziki vichaa waliokomaa vichwa!uongo mbaya ! jamaa shughuli wanaiweza na wanaipeperusha bendera kisawa sawa,vichaa mnakubalika

  2. kikosi hiki cha ffu wa Ngoma Africa nawapenda mziki wao kwani ni wanamziki wenye kujituma na kutingisha kimataifa

Post a Comment