KIMWANA IRENE UWOYA KUCHUKULIWA JUMLA MWEZI AGOSTI!!

Kimwana Irene Uwoya katika Pozi.

Mwigizaji maarufu wa Filamu na mwenye mvuto zaidi hapa nchini aliyewahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania na kushika nafasi za juu katika shindano hilo kubwa la Urembo nchini kimwana Irene Uwoya, ameimabia FULLSHANGWE hivi karibuni kwamba anatarajia kufunga ndoa yake na mwanasoka Hamad Ndikumana kutoka nchini Rwanda mwzi wa nane.

Irene Uwoya aliiambia FULLSHANGWE kwamba mambo yote na taratibu zingine za kimila zimekamilika kinachoendelea kwa sasa ni maandalizi ya ndoa hiyo ambayo amesema itafungwa hapahap Bongo na mwandani wake huyo.

Mchumba wake huyo Hamad Ndikumana kwa sasa yuko nchini Cypruss ambako anacheza soka la kulipwa katika timu ya Omonia ya huko, mara mipango itakapokuwa imekamilika atakuja hapa nchini kwa ajili ya kufunga ndoa na mchumba wake,

Irene amesema yanasemwa mengi lakini yeye ameshafika na ameamua hivyo hageuki nyuma kwa kuwa anampenda mchumba wake huyo na wana mipango ya mambo mengi ya maisha mara watakapoanza kuishi pamoja kama mke na mume baada ya ndoa yao kufungwa rasmi hapo baadaye mwezi wa nane.

FULLSHANGWE inawatakia kila baraka katika mipango ya kufunga ndoa yenu na mungu awabariki iweze kufanikiwa kama ilivyopangwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment