Dr. Joseph Kahamba ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya Ubongo, Uti wa mgongo na Mishipa ya Fahamu akiongea na waandishi wa habari, baada ya kuagana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda aliyekwenda hospitalini hapo jioni hii, kumjulia hali Dr Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela Mjini CCM aliyelazwa katika kitengo cha mifupa MOI Hospitali ya Muhimbili kutokana na ajali aliyopata mkoani Iringa, kijiji cha Ihemi wakati akirejea Jijini Dar es alaam akitokea mkoani Mbeya, Dr. Kahamba amesema Dr. Mwakyembe anaendelea vizuri na hakuna haja ya kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi kwa kuwa hajaumia sana na wala hajavunjika popote mbali ya maumivu na majeraha ya kawaida wakati mtu anapopata ajali na gari ikaharibika vibaya kutokana na misuguano na mitikisiko mkubwa inayotokea wakati wa ajali hata hivyo kazi ya kupiga picha ilikuwa ngumu sana kwa wapiga picha wa Televisheni na magazeti kutokana na sababu za kiusalama na chumba alicholazwa mgonjwa kuwa kidogo hivyo aliruhusiwa mpiga picha mmoja tu kutoka Ofisi ya Waziri mkuu.
Hapa Mh. Waziri mkuu akiongozana na Dr. Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu Dr Joseph Kahamba kushoto wakati alipowasili katika Kitengo cha mifupa MOI Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokwenda kumjulia hali Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela Mjini CCM kutokana na majeraha ya ajali aliyopata juzi mkoani Iringa.

Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akiondoka katika kitengo cha mifupa cha MOI kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jioni hii alikokwenda kumjulia hali Mbunge wa jimbo la Kyela Mjini Dr. Harrison Mwakyembe aliyelazwa Hospitalini hapo kutokana na majeraha ya ajali aliypata kutokana na ajali iliyotokea Mkoani Iringa katika kijiji Cha Ihemi Juzi baada ya gari aliyokuwa akisafifira kupasuka gurudumu la mbele na kupinduka Dr. Mwakyembe alikuwa akitokea Mkoani Mbeya kurejea Dar es alaam.
0 comments:
Post a Comment