VIDEO ZA FEISAL ISMAIL NA BABY MADAHA KUZINDULIWA MEI 30 KILIMANJARO KEMPINSKI!!

Mkurugenzi wa Uzalishaji wa kampuni ya Pili-pili Entertainment ya jijini Bw. Nilesh Bhatt akionyesha Albam mbili za Feisal na Baby Madaha wakati alipozungumza na wanahabari juu ya uzinduzi wa Albam hizo Mei 30 katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kulia ni Sofia Mdecha Meneja Matukio wa Pili-pili Entertainment.

Video kali na za kuvutia zilizotengenezwa katika mahadhi ya utamaduni wa India na Tanzania za wasanii wa muziki wa kizazi kipya Baby Madaha na Feisal Ismail zimekamilika, na ziko mbioni kuanza kurushwa katika vituo mbalimbali nchini na nje ya nchi kutokana na ubora wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa uzalishaji wa kampuni ya Pili-pili Entertainment iliyosimaia kazi nzima ya kurekodi video hizo Bw. Nilesh Bhatt amesema wamefanya kazi nzuri itakayowafanya wasanii hawa kutambulika zaidi nje ya nchi yetu yakiwemo mabara tofauri ya bara la Afrika na Asia kutokana na kurekodi video zao na wasanii wa Bollwood India kitu ambacho kinaukutanisha utamaduni wa India kutoka Bara la Asia na Tanzania kutoka Bara la Afrika kufanya kazi pamoja.

Ameongeza kuwa Video hizo zinatarajiwa kuzinduliwa mwezi huu Tarehe 30 katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski sambamba na kuizindua Kampuni ya Pili-pili Entertainment, ambapo mgeni rasmi atakayezindua atakuwa mama Dr. Mary Nagu Waziri wa Viwanda na Biashara na mara baada ya uzinduzi huo kuna vipindi maalum vitarushwa katika Televisheni mablimbali ili Watanzania washuhudie uzinduzi huo.

Baada ya uzinduzi huo wa Mei 30 yatafuatia maonyesha yatakayofanywa na wasanii hao karibu nchi nzima wakianzia mikoa ya Dar es alaam, Mwanza na Arusha na baadae watavuka mipaka na kufanya maonyesho mengine katika Afrika Mashariki kwenye majiji ya Kampala Uganda na Nairobi nchini Kenya

Ameongeza kuwa Albam hizi zimerekodiwa kwa pamoja na wasani wengine kamaPancho Latino Chid Benzi, Nura, Mr. Blue na Feri Kano, ambapo albam ya Baby Madaha inalenga katika Mapenzi na Albam ya Fisal inalenga katika mambo ya kutumaini mafanikio, ameongeza kuwa wimbo wa Baby Madaha unafundisha kwa kiwango kikubwa, kwani zaidi ya miaka 50 iliyopita Utamaduni wa India ulikuwa umejifunga sana lakini kwa sasa unaanza kufunguka na kuingiliana na tamaduni nyingine nyingi, hivyo mabadiliko yataanza kutokea kadiri siku zinavyoenda na nyimbo hii ya Baby hakika itakuwa ni Fundisho zuri kwa jamii za watu wa nchi zote mbili yaani India na Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment