MISS IFM KUPATIKANA MEI 15 IJUMAA MSASANI CLUB!!

Kuanzia kulia ni Peter Sarungi Mwenyekiti Miss Ifm, Lazaro Lutobeka Mjumbe na Frorence Josephat Mwalimu wa warembo wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo pale Break PointOutdoor Posta.
Warembo watakaoshindania taji hilo wakipozi kwa picha.

Shindano la kumsaka Miss Ifm 2009 linatarajiwa kufanyika ijumaa wiki hii tarehe 15 Mei katika ukumbi wa Msasani Club jijini, hayo yamesemwa leo na mwenyekiti wa kamati inayoandaa shindano hilo Bw. Peter Sarungi katika ukumbi wa Break Point Posta leo wakati alipozungumza na vyombo vya habari kuhusiana na shindano hilo.
Sarungi amesema tayari warembo wengi wameshajitokeza ili kushiriki katika shindano hilo ambalo litakuwa ni la pili kwa upande wa mashindano ya urembo katika vyuo vya elimu ya juu, amewataja warembo wanaoendelea na mazoezi kwa ajili ya shindano hilo kuwa ni Witness Boaz, Beatrice Lukindo, Diana Mhenga, Francisca Mansilo, Jesca Mhagama, Easther Gao, Anneth Brayson,Veronica Micky,Evon John, Elvira Jacob Ratifa Mhamed na Arvia Rashid.
Ameongeza kuwa mshindi wa kwanza katika shindano hilo ataibuka na kitita cha shilingi 500.000 mshindi wa pili atapata shilingi 350.000 wa tatu atapata shilingi 200.000 na mshindi wa nne na kuendelea watapata shilingi 100.000 kila mmoja.
Wadhamini wa wakuu shindano hilo wametajwa kuwa ni Vodacom wakisaidiana na Chanel Ten, Clouds Entertainment, Mwasu Fashion, Merry Rose Cosmetics, Break Point OutDoor Ltd,KP Fashions na Nice Magazine.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment