SHANI ANTONY AUKWAA U- MISS VODACOM KURASINI 2009!!

Miss Vodacom Kurasini 2009 Shani Anthony akipunga mikono kwa mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi, katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni, kushoto ni mshindi namba mbili Celina Chipeta na kulia mshindi wa tatu Irene John.

Mkurugenzi wa Miss Tanzania akiangalia pini zake mara maada ya kutangazwa kwa mshindi Shani Anthony akifuatiwa na Celina Chipeta kushoto na Irene john kulia.
Tano Bora ya Miss Kurasini kuanzia kulia ni Christina Thomas Irene John, Shani Anthony,Cathe Paul na Celina Chipeta wakiwa katika picha ya Pamoja.
Hapa hakuna mchezo lazima mfanye kazi ambayo itatuletea warembo bomba kwa ajili ya Miss Tanzania na mwakilishi wetu Miss World sio kila wakati tuchemshe tu inaelekea Hashim Lundenga Mkurugenzi wa Miss Tanzania aliyesimama nyuma ya majaji, ndivyo alivyokuwa akiwambia majaji wa shindano hilo wakati wa mchakato wa kuwapata washindi.

Kundi la Diamond Musica likiwa jukwaani likifanya vitu vyake vikubwa wakati wa shindano la kumtafuta Miss Vodacom Kurasini usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Equator grill Mtoni.

Wanne Star Msanii machachari wa ngoma za asili alikuwepo na rafiki yake kama unavyowaona wakifuatilia kwa karibu shindano hilo.


Kiongozi wa Bendi ya Diamond Misica liver Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wanenguaji wa Bendi hiyo wakati kundi hilo lilipotumbuiza kwenye shindano la kumtafuta mlimbwende wa kitongoji cha Kurasini kanda ya Temeke usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment