MAMA SALMA KIKWETE AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGIA ELIMU KWA WATOTO WENYE ULEMAVU!!

Meneja Uhusiano wa Benki ya Starndard Chartered Hoyce Temu akipokea tiketi ya ndege ya kwenda HongKong na Kurudi Dar, aliyoinunua kwa Dolla za Kimarekani 2500 kutoka kwa Mgeni rasmi mama Salma Kikwete wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wenye ulemavu iliyofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jana
Jumla ya shilingi milioni 266.5 zilipatika ikiwa ni fedha taslimu , vifaa na ahadi, hafla hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Elimu Nchini (TEA) na kuendesha na Mke wa Rais mama Salma Kikwete, hata hivyo Hoyce Temu alikabidhi tena tiketi hiyo kwa mama Salma Kikwete ili inadiwe tena katika kuongeza zaidi mapato ya Harambee hiyo.
Mgeni Rasmi mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi na wadau mbalimbali wa Mamlaka ya Elimu Nchni TEA.
Meneja masoko wa Multchoice Furaha Samalu kushoto akiwa pamoja na Mustafa Hassanali katika harambee hiyo.

Kuanzia kulia Mbunifu Zamda George, Mrembo Angela Damas, Jaquiline Ntuyabaliwe ambaye kwa sasa ni mwanamuziki akijulikana kama Kylin na mbunifu wa mavazi kutoka Zanzibar Farouk Abdella wakitoa mawili matatu mbele ya mgeni rasmi mama Salma Kikwete mara baada ya kuonyesha nguo zao.

Hoyce Temu akipita na Vazi lililobuniwa na Mustafa Hassanali, vazi hilo limetengenezwa kwa khanga kama unavyoliona.

Jaquiline Ntuyabaliwe a.k.a Kylin akipita na vazi lililobuniwa na mbunifu wa mavazi kutoka Zanzibar Farouk Abdella wakati warembo mbalimbali walipoonyesha nguo zilizobuniniwa na wabunifu wa mavazi wa hapa nyumbani, ili zinadiwe kwa ajili ya kuchangia mfuko wa elimu unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Nchini (TEA), nguo hizi zilionyeshwa jana katika harambee iliyofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick Mgeni rismi akiwa Mama Salma Kikwete.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment