Hapa wanamitindo wakipita jukwaani kwa pamoja mara baada ya kukamilisha kuonyesha nguo katika Onyesho la Delectable Fashion kwenye Hoteli ya movenpick jana, hakika lilikuwa ni onyesho lililotoa somo kwa wabunifu wa nyumbani kutokana na kazi za mbunifu kutoka uganda Madoi Latif aliyeonyesha nguo mbalimbali zikiwemo za kutokea, michezo nguo zinazopendwa kuvaliwa na vijana zaid na nguo za kijeshi , kimsingi mimi niliona tofauti kidogo na maonyesho mengine ambayo tumekuwa tukiona karibu kitu kilekile japokuwa nguo zinakuwa nzuri sana, lakini tatizo mitindo ya nguo zao haibadiliki sana ukilinganisha na onyesho la jana ambalo nguo nyingi zilikuwa na ubunifu tofautitofauti, kwa matukio zaidi mdau wa FULLSHANGWE shuka chini upate uhondo wa mavazi ya Ally Rehmtullah na Madoi Latif.
Hapa ikafika zamu ya Mwenye Shughuli yaani Ally Rehmtullah na Delectable Fashion yake iliyokuwa na vivazi vya aina yake wakati vilipokuwa vikonyeshwa jukwaani.
Hapa ikafika zamu ya Mwenye Shughuli yaani Ally Rehmtullah na Delectable Fashion yake iliyokuwa na vivazi vya aina yake wakati vilipokuwa vikonyeshwa jukwaani.
Vazi la Jioni
Huyu siyo Askari wa Obama kule Irak hapana ni mwanamitindo akionyesha moja ya mavazi ya kijeshi yaliyobuniwa na mbunifu wa Uganada Madoi Latif.
Cheki hivi viatu vilivyobuniwa na Madoi Latif kutoka Uganda.
Hapa sasa ndipo vilipoanza kuonyeshwa vitu vikali vya mbunifu Madoi Latif kutoka Uganda, huyu alionyesha uwezo mkubwa katika kutengeneza nguo zake, hebu jaribu kuangalia baadhi ya picha ujionee mwenyewe yuko katika kiwango gani ukilinganisha na wabunifu wa mavazi hapa nyumbani.
THT nao walitisha kwa uwezo wao wa kutisha katika sanaa hii ilikuwa ni burudani tosha wadau wa FULLSHANGWE wakati mwingine ukiwasikia THT jaribu kwenda kuwaona ili ujionee mwenyewe jinsi wanavyoiweza sanaa ya muziki kwa sasa hapa nchini.
Kundi la sarakasi la Mama Africa likifanya mambo makubwa kabla ya onyesho hilo kuanza
Mkalia wa Filamu nchini Kanumba kushoto na rafiki yake nao wakajiachia kama kawa.
Aunt, Matukio chuma Fiderin Ilanga na fatma Hassan nao hawakubaki nyuma kwa mapozi jamani.
Wabunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka na Mustafa Hassanali wakipiga makofi ili sikujua kitu gani kilichowavutia sana katika onyesho hilo la mavazi lililokuwa zuri.
Maadam Juliana akiwa na Miss Tanzania 2007 Richa Adhia na Jaquiline wa duka la nguo Jaq Boutique liloko Namanga wakifuatilia kwa karibu kila kilichojiri katika onyesho hilo.
Washabiki na wapenzi mbalimbali wa mitindo ya mavazi waliohudhuria katika onyesho hilo wakishangilia na kupiga makofi wakati kundi la THT ilipokuwa likitumbuiza Jukwaani.
0 comments:
Post a Comment