Yule msichana wa Romania Alina Percea aliyatangaza kuiweka bikira yake kwenye mnada nchini Ujerumani miezi michache iliyopita amefanikiwa kupata mteja baada ya mnada huo kuisha na mwanaume mmoja raia wa Italia kufikia dau la euro 10,000.
Alina Percea mwenye umri wa miaka 18 aliinadi bikira yake kwenye tovuti moja nchini Ujerumani miezi michache iliyopita.Alina alipanga kuzitumia fedha atakazopata baada ya kuuza bikira yake kwaajili ya kujisomeshea chuo kikuu na kuisaidia familia yake masikini iliyopo nchini Romania.Mnada huo ulifikia tamati siku ya alhamisi kwa Muitaliano mmoja ambaye hakutajwa jina lake kuibuka mshindi katika dakika za mwisho mwisho za mnada huo."Nasubiri kwa hamu, nilifikiri dau lingepanda juu zaidi lakini hata hivyo nina furaha" alisema Alina.Alina aliwasili Mannheim, Ujerumani mwezi januari akitokea kwao Romania na aliamua kuingia kwenye mnada huo baada ya kushindwa kupata kazi.Mnada huo uliingia dosari wiki tatu zilizopita baada ya mwalimu wa shule ya zamani ya Alina kudai kuwa Alina sio bikira.
Hali hiyo ilipelekea Alina ambaye kabla ya mnada huo alipimwa bikira yake, ilimbidi afanyiwe majaribio kwa mara ya pili kuthibitisha bikira yake.Daktari aliyemfanyia majaribio hayo alitangaza katika kikao na waandishi wa habari kwamba "Alina kweli ni bikira na hajawahi kufanya mapenzi".
Alina aliamua kuinadi bikira yake baada ya kuona mafanikio aliyoyapata mwanafunzi wa Marekani Natalie Dylan mwenye umri wa miaka 22 ambaye alipata mteja wa bikira yake aliyoinadi kwenye tovuti moja nchini humo aliyefikia dau la dola milioni 3.5." Hakuna mtu aliyeniambia nifanye hivi, ni matakwa yangu binafsi" alisema Alina."Sijui ni lini au wapi nitakutana na mshindi wangu, lakini nafurahia kusafiri iwapo atalipia gharama za usafiri"."Tutaenda hotelini katika wiki chache zijazo na tutatumia usiku mmoja pamoja, na kama tukipendana tunaweza tukakaa pamoja na usiku wa pili"."Tunaweza tukatumia kondomu au kama atafanyiwa vipimo vya magonjwa ya zinaa niko tayari kumeza vidonge vya kuzuia mimba"."Natumaini jamaa ataelewa kuwa mimi ni bikira hivyo atanihudumia vizuri" alimalizia kusema Alina. (Kimbwanga hiki katutumia mdau James Biboze wa Holland)
0 comments:
Post a Comment