MR. PAUL "NARUDI TANE KWENYE MUZIKI"


Mwanamuziki mtanzania Paul Mbena aka Mr Paul amerudi kwenye uringo wa muziki kama alivyoahidi nilipofanya mahojiano na Mtandao wa Spoti na Starehe mara ya mwisho.
Paul ambaye kwa sasa anaishi na kufanya shughuli zake za kimuziki nchini Australia kwenye jiji la Melbourne anasema kuwa ameshakamilisha nyimbo mbili ((Nakutamani na Malaika wa Moyo wangu) ambazo ziko kwenye mtindo wa Afro Funk style, nyimbo hizi ndizo zitakuwepo kwenye mradi wa Multicultural Art Victoria Visible CD, mradi ambao unajumuisha wanamuziki wa mataifa na mitindo mbalimbali (Gonga hapa kusoma zaidi.) angalia page ya mwisho utaona nafasi ya Paul Mbena ambaye kwenye mradi huu ametambulishwa kama Project Officer.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment