Haya sasa huyu ndiyo Beatrice Lukindo Miss Vodacom IFM 2009, Kimwana atakayewakilisha chuo hicho katika mashindano ya kanda ya Vyuo vikuu yatakayofanyika mwezi juni, mlimbwende huyu amepatikana katika shindani lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Msasani Club jijini Dar na kuibuka na kitita cha shilingi laki 500.000 taslimu na zawadi zingine kutoka maduka ya nguo ya KP Mdau pata matukio mbalimabli katika picha juu ya yaliyojiri katika shindano hilo lililokuwa zuri tulivu na la kuvutia.
Miss Vodacom IFM Beatrice Lukindo akiwa pamoja na washindi wenzake, wakipozi kwa picha na mwandaaji wa Miss Highlearning na aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo Manka Mushi kushoto na kulia ni George Rwehumbiza Meneja Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Miss Vodacom Tanzania.
Hapa washindi wa Miss Vodacom IFM wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo mara baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Msasani Club.
Miss Vodacom IFM Beatrice Lukindo akiwapungia mkono mashabiki wake mara baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumtafuta mrembo atakayewakilisha chuo cha IFM katika shindano la Miss Vodacom Highlearning linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao kushoto ni mshindi wa pili Esther Gao na kushoto ni mshindi wa tatu Veronica Micky.
Hapa wakiulizwa maswali tayari kwa kuwapata washindi wa Miss Vodacom IFM na kulia ni Jaji mkuu Manka Mushi akiwasomea maswali warembo hao.
baada ya kupita na vazi la jioni hawa ndiyo warembo walioingia Top Five ya Miss Vodacom IFM kutoka kushoto ni Beatrice Lukindo, Esther Gao, Veronica Nicky,Annet Brayson na Francisca Mansilo.
QJ kushoto na Makamua wakikileta shangwe kwa mashabiki na wapenzi mbalimbali wa Urembo waliohudhuria katika shindano la Miss Vadacom IFM liliofanyika jana Msasani Club.
Msanii Noora kati akifanya vitu vyake na kundi lake la Chamber Squard Msanii huyo pia anasoma katika chuo cha IFM.
hapa walikuwa wakipita na Vazi la ubunifu.
Hapa sasa ndiyo mambo yanaanza kama unavyoona warembo wakifungua rasmi shindano lao kwa showa kabambe iliyochezwa maridadi na warembo hao.
Mwalimu lazima ajue pozi jamani wadau wa FULLSHANGWE si mnaona wenyewe pozi la Mwalimu wa warembo Miss Frolence kutoka IFM.
Masoud Kipanya kulia Hee jamani Stella ndiyo pozi gani tena hizo jamani Mh!! Ngoja na mimi niweke pozi langu la Ki MaishaPlus tuone kama utanishinda.
Mgeni wa heshima Naibu meya wa jiji la Dar es alaam Ahmed Mwilima akifungua rasmi shindano la Miss Vodacom IFM katika ukumbi wa Msasani Club jana kulia ni Meneja Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza na kushoto ni Mmwenyekiti wa kamati shindano hilo Peter Sarungi.
Evance Bukuku wa Eventlight akiwa na marafiki zake wakiteta jambo, kwenye burudani kuna mambo mdau!
Majaji wa shindano hilo kuanzia kulia ni jaji mkuu na mwandaaji wa Miss Vodacom Highlearning Manka Mushi, Sam Mshana, Evance, Nana Philipna Silvestre Mlimi wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
Mgeni wa heshima kushoto ambaye pia ni Naibu Meya wa jiji la Dar es alaam Ahmed Mwilima akizungumaza na Meneja udhamini na Mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza kati na Msaidizi wa Meya huyo, Mwisho kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Miss IFM Peter Sarungi wakati wa shindano la Kumsaka mrembo wa Miss Vodacom IFM jana pale Msasani Club.
0 comments:
Post a Comment