JIKHOLABWINO APAGAWISHA TAMASHA LA KUMKUMBUKA BOB MARLEY!!

Jhikolabwino Siza Manyika Jikhoman) akikug'uta gitaa la sollo vilivyo, kwa sasa naweza kusema hakuna mwanamuziki wa muziki huo ambaye anamfikia Jikhoman na kundi lake la Afrikabisa katika muziki wa Reggae hapa nchini kwa sasa , manake jinsi alivyokuwa akiwarusha mashabiki wake usiku wa kuamkia leo, kusema kweli ni tamasha lililonivutia sana na nilikumbuka nyimbo nyingi za Bob Marley nilizokuwa nikizisikiliza tangu miaka ile.

Hata hivyo kilichonisangaza katika tamasha hilo, ni kuwa kama nilivyozoea katika matamasha mengine kuona Counter ziko Busy, kila mtu anajinunulia kinywaji chake yaani "Ze Lager" au "Grants" au kinywaji kingine chochote, lakini jana ilikuwa tofauti sana japokuwa waliokuwa wakipata Ze Lager walikuwa wachache, niliowaona wengi wao walikuwa na chupa za soda au maji, kilichonishitua zaidi nilihisi Harufu kali na moshi ukiwa unatanda angani! ah lakini nikakumbuka kuwa siku mbili zilizopita bado mabomu yalikuwa yakilipuka kule mbagala Jeshini,
Hivyo nikafikiri kuwa huenda bado kulikuwa na mabaki ya moshi wa mabomu hayo ambao huenda ndiyo umetanda katika ukumbi huo, manake nilishindwa hasa kuielewa harufu ile ilikuwa ni ya nini na ilikuwa ikitoka wapi japokuwa nilikuwa naona watu wengi wanavuta sigara ambazo sikuzitambua majina yake manake ilikuwa usiku hivyo ilikuwa ngumu pia maandishi yake kusomeka kirahisi, Ah hata hivyo nikaona ngoja niachane na habari hizo manake kila mtu ana starehe yake mdau wangu hebu tuache kama ilivyo.

Jhikolabwino na kundi lake wakifanya mambo makubwa katika tamasha hilo lililoandaliwa na kipindi maarufu cha muziki wa Reggae cha Caribbean Beat kinachorushwa na Radio Clouds Fm kikiendeshwa na mtangazaji Benji Cosmo.

Hapa wameshabanjuka na muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kundi maarufu la Reggae kwa sasa Afrikabisa linaloongozwa na mwanamuziki Jhikolabwino Siza Manyika (Jhikoman).

Mashabiki na wapenzi wa Mwanamuziki wa Reggae kutoka Jamaica Robert Nesta Marley maarufu kama Bob Marley wakiselebuka wakati wa onyesho maalum la kumkumbuka llililofanyika jana kwenye ukumbi wa Ghanzhou Chinese Garden jijini Marley alifariki miaka 28 iliyopita lakini bado anakumbuka kutokana na muziki wake kuigania haki za binadamu na uhuru wa Mwafrika duniani kote.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment