Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM Bw. John Ngowi ambaye pia ni mpiga debe wa mgombea urais wa Serikali ya wanafunzi chuoni hapo Bernard Lupungu, amebuni mbinu mpya ya kumpigia debe mgombea wake kwa kuvaa picha zake karibu kila mahali katika mwili wake na mkoba wake wa madaftari, Ngowi amesema anasimama kidete kumpigania debe Bernard Lupungu mpaka atakapokamata madaraka ya kuongoza serikali ya wanafunzi chuoni hapo, kama unavyomuona hapa akiwa katika hekaheka za kupiga kampeni huku na kule jamani wadau kampeni si mchezo.
HII NDIYO MBINU MPYA YA KAMPENI ZA URAIS IFM!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment