MISS TANZANIA ASHEREKEA KUZALIWA KWAKE NA WATOTO YATIMA!!

Hapa watoto wakipata mlo saafi ulioandaliwa na Hoteli ya Giraffe Ocean View kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa kwa Miss Tanzania Nasreem Karim iliyofanyika leo Hotelini hapo watoto yatima kutoka vituo mbalimbali walijumuika pamoja na Nasreem na kula chakula hicho pamoja na mrembo huyo na kucheza michezo mbalimbali,vituo hivyo ni Makuya Orphans and Vulvarable Children, Sinza orphanage Children Centre, Nira Children and Youth Orphans Foundations na Unra Orphanage Centre vyote vya jijini FULLSHANGWE tunampongeza Nasreem kwa kusherekea kuzaliwa kwake na watoto yatima tunasema heko na endelea na moyo huo.
Miss Tanzania Nasreem akiwasaidia watoto kuchukua chakula.

Watoto wakiwa wamezunguka keki tayari kwa kukata Pamoja na Miss Vodacom Tanzania Nasreem Karim leo kwakweli watoto walifurahi na walijisikia vyema kula chakula pamoja na miss Tanzania.

Miss Vodacom Tanzania Nasreem Karim akicheza na watoto katika sherehe ya kuzaliwa kwake iliyofayika katika hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko Mbezi Beach leo Nasreem amesherekea kuzaliwa kwake na kula chakula pamoja na watoto yatima kutoka vituo mbalimbali jijini.

Kikundi cha burudani Chiwawa kikitoa burudani kwa watoto huku wakishangilia kwa furaha na kupiga makofi.

Meneja mkuu wa Giraffe Ocean View Hotel Bw. Rahool kushoto akifanya mahojiano na wakuu wa kitengo cha matangazo cha Star Sport Magazine Al hadji Hassan Mnyenye kati na Mohamed wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa na Hoteli hiyo kwa ajili ya Miss Vodacom Tanzania Nasreem Karim kula pamoja na watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao jijini katika sherehe ya kuzaliwa kwake leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment