Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mara mbaada ya kuzindua na kutembelea maabara ya kisasa iliyojengwa kwa hisani ya shirika la Kimarekani la Abbott Fund katika Hospitali ya Amana leo na hii ni maabala ya kwanza kati ya maabala kadhaa zilizoahidiwa na shirika hilo kwa Tanzania.
Makamu wa Rais wa Abbott Fund Christy Wistar akimpa maelezo waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa aliyesimama kulia wakati alipotembelea maabara ya kisasa iliyojengwa kwa masaada wa shirika hilo katika Hospitali ya Amana mara baada ya uzinduzi leo asubuhi katikati ni meneja wa Maabara hiyo Costantine Mzava na mwenye kofia ni Mussa Azan Zungu Mbunge wa jimbo la Ilala.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akikata utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi wa maabara ya kisasa katika Hospitali ya Amana iliyojengwa kwa msaada wa Abbott Fund shirika linalotoka Marekani waliosimama kutoka kulia ni Christina Mwangi Prog. Chief Surport CDC Tanzania, Vice President Abbot Fund Christy Wistar na waliosimama kutoka kushoto ni Mganga mkuu wa Hospitali ya Ilala Dk. Willy Sangu na Dafrosa Lyimo Mganga mkuu wa Wilaya ya Ilala.
Mwandaaji wa uzinduzi huo Matina Nkurlu kushoto akizungumza na mmoja wa wageni waliokuwepo katika uzinduzi huo aliyekuwa akipiga picha tukio hilo FULLSHANGWE haikufanikiwa kunasa jina lake mara moja lakini ilivutiwa na uratibu wake jinsi alivyokuwa akipanga mikakati ya upigaji picha wakati wa zoezi hilo ili kuhakikisha matukio yote yanapatikana katika kumbukumbu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maabara ya kisasa iliyojengwa kwa msaada wa shirika la Abbott Fund la Marekani Prof. David Mwakyusa akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Makamu wa rais wa Abbott Fund Tanzania Bi. Christy Wistar akizungumza katika uzinduzi huo ambao ulifanyika katika Hospitali ya Amana.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Amana Dk. Willy Sangu akiongozana na waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Azan Zungu kwenda kuzindua rasmi maabara hiyo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa wamekaa tayari kwa kushuhudia uzinduzi huo.
Brass Band ya Polisi ikifanya vitu vyake kabala ya kuanza rasmi kwa shughuli za uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyojengwa katika Hospitali ya Amana kwa msaada wa shirika la Kimarekani la Abbott Fund nchini leo jijini ambapo waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa.
Brass Band ya Polisi ikifanya vitu vyake kabala ya kuanza rasmi kwa shughuli za uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyojengwa katika Hospitali ya Amana kwa msaada wa shirika la Kimarekani la Abbott Fund nchini leo jijini ambapo waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa.
1 comments:
Ahsanteni kwa maabara ya kisasa hospitali amana, labda itatupunguzia gharama ya nauli na usumbufu wa muhimbili kwa sisi wakazi wa ilala na vitongoji vyake.
Mwisho naomba nimkumbushe mheshimiwa ZUNGU, "ZUNGU, TUNATAKA BARA BARA YETU ULIYOTUAHIDI SHINGOFENI TUMECHOKA KUOGELEA WAKAKI WA MVUA, UWIIII! TUKWAMBIE VIPI HUSIKII?!"
Post a Comment