Vencha alinifurahisha sana na kivazi chake cha msuli, vazi hili ni maarufu sana kwa wakazi wa ukanda huu wa Pwani, hapa akiita wateja kwa ajili ya kununua mitumba yake maarufu kama (Ronya) huko mtoni Wilayani Temeke.
Wakazi wa jiji bado wako katika mazingira hatarishi yanayoweza kupelekea maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine kutokana na kufanya biashara zao katika mazingira yasiyo salama kama alivyokutwa mchuuzi huyu wa mishikaki ya kuchoma ama (nyamachoma) akiwauzia wateja wake nyama hiyo katika maeneo ya Mtoni Mtongani jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment