Combine ya longtime tu toka kitaa 'Makavu live' inakuja rasmi na tayari jamaa wameshaachia nyimbo inayowatambulisha vizuri tu inayoitwa ONGEA MWANA iliyotayarishwa na producer Vil wa V nice production, studio ambayo ilivamiwa na majambazi siku za hivi karibuni. Makavu live imeundwa na wasanii 5 wa muziki wa kizazi kipya ambao ni Omary Muba'Omy G', Abraham Kasembe'Dullayo', Xavier Renne 'Xdizo', Pompin na Isihaka Salehe 'Eazy man'.
Jamaa walikua wanakutana maskani mitaa ya ukonga huko pande za airport wakawa wanachanana kwa ma-freestyle makalimakali ambayo walikua wanayaita makavu, ndipo walipopata familia yao iliyo batizwa jina la makavu live.
Tayari wameshafanya nyimbo nyingi tu za bongofleva mpaka za mnanda zilizotengenezwa na maproducer tofauti hapa jijini. Wanasema " kiparatuni chetu kinatusaidia sana hasa kubadilishana uzoefu katika sanaa kwani kuna wasanii kibao wenye style na skills tofauti tofauti, Mungu atatusaidia familia itakua na
tutaibua wasanii wengine wenye vipaji vilivyojificha".
Yupo mwana hiphop mkongwe, Omy G msanii mwenye sauti ya pekee aliyetoka tangu mwaka 2000 na nyimbo ya 'kindumbwendwe'akiwa na kundi la FDC, kwasasa alitoa nyingine inayoitwa 'choo cha kike'kabla ya kuachia 'Skiliza mchumba' aliyomshirikisha Dullayo, mwingine ni Dullayo anae-shine sana na 'bila yule'
akimshirikisha Mwana-Fa, pia yupo Xdizo alieachia kali yake inayoitwa 'Dhahabu zilizopotea' ikitengenezwa na Marco Chali bila kumsahau Pompin mkali wa freestyle na Eazy man anae-shine sana kwenye nyimbo yao ya mnanda inayoitwa 'maneno wapi'.
Pamoja na kuwa wapo kwenye kundi moja kila msanii yuko huru na anaendelea kusuka albam yake bila kuadhiri muungano wao. Sasaivi wapo katika mchakato wa kutangaza muungano wao, wanapiga picha za pamoja na video ya nyimbo zao mpya.
1 comments:
Kila la kheri masela, umoja ni nguvu msitengane!
msije kua km wanaume tmk, ect na wenginewengine yani msilale ila poa sana kuungana!!!!!!!!!
Post a Comment