Habari zilizoenea zinasema yule mwanaume aliyejibadilisha jinsia na kuwa na maumbile ya kike Abdalla Alou a.k.a (Aunt Victoria) aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala na baadae kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili amefariki dunia.
Habari zilizotufikia kutoka Hospitalini hapo zinasema mwanaume huyo alifariki leo baada ya kuzidiwa, inadiwa kwamba mwanamume huyo hapo zamani alikuwa na nyumba ya urithi iliyokuwa maeneo mbezi
Jamaa huyo aliamua kuiuza nyumba yao na kueleke nchini China ambako alifanyiwa upasuaji wa kubadilishi maumbile yake ya siri kutoka mwanaume na kuwa mwanamke, baada ya upasuaji huo aliendelea kuishi huko China na Thailand katika jiji la Bangkok.
Baada ya kuona hali yake ya kiafya imezorota alirejea nyumbani Tanzania ambapo haikuwa nzuri inadaiwa kuwa mtu huyo aliokotwa na polisi wa kituo cha kawekubakwa na kutelekezwa ndipo alipolazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, ambapo baadaye alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili ambako ndiko alikofia, inakadiriwa kuwa (Aunt Victoria) alikuwa na miaka kati ya 35 na 45 japokuwa yeye alipohojiwa wakatia akiwa hospitali baada ya kuzinduka alidai kuwa na miaka 70. Tutawaletea Habari zaidi kutokana na mkasa huo Baadae
0 comments:
Post a Comment