PINI ZA MISS VODACOM KURASINI ZAENDELEA KUJIFUA!!



Mazoezi ya warembo watakaoshiriki kinyang'anyiro cha kumtafuta Miss Kurasini 2009 yanaendelea katika ukumbi wa Equator Grill Mtoni, ambapo jumla ya warembo 14 wanashiriki.
Mwanadaaji na mkurugenzi wa kampuni ya Zum Fashion and Entertainament Zuwena Mustafa amesema shindano hilo linafanyika katika ukumbi wa Equator Mei 23 Jumamopsi ili kuwapata wawakilishi watatu watakaowakilisha kituo hicho kwenye shindano la Kanda ya Temeke, na hatimaye tukifanikiwa Miss Vodacom Tanzania.
Amewataja warembo waliojitokeza kuwa ni Grace Msangi, Memus Ruth, Selina Kapeta, Annamaria Marcelli, Kibasu Paulo, Christina Thomas, Mary Salum Jacquiline Steven, Leticia Joseph, Shani Kimambo, Anipha Daudi, Nuru Mohamed, Irene John na Khadija Shaban.

Watakaoporomosha Burudani ni Bendi ya ni Diamond Musica, watakaoshirikiana na kundi la Taarab la Coast Molden Taarab na mwimbaji maarufu wa muziki wa taarab Mwanahawa Ally ambapo kiingilio kitakuwa kati ya shilingi 10.000 na 5000,

Shindano hilo linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom, Redds Premium Cold, Big Solutions, Afro World Saloon na Pijei

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment