MDAU AANZISHA BLOG YA KIBIASHARA, HEBU MTEMBELEE!!

Hatimaye Watanzania sasa wanaweza kuchati kibiashara kwa kupitia blog mpya ya fani za masoko na biashara.
Mwanzislishi wa blog hiyo anaitwa Allan Rwechungura na anaitaja blog yake kuwa inaitwa
http://tzads.blogspot.com
Mwanzilishi huyo amesema bog yake iko hewani kuanzia jana.
Amesema blog hiyo ambayo ni ya kibiashara ina lengo la kuwashirikisha wadau wa masuala ya masoko na biashara kubadilishana mawazo kuhusiana na fani hiyo.
"Hii blog ipo kwa watu wote wenye mawazo chanya na ambayo pia mbali na matangazo ya kibishara itajihusisha na mijadala mbalimbali katika fani ya masoko na biashara," alisema.
Amefafanua kwamba fani ya masoko na biashara ni moja ya fani zinazoheshimika hapa nchini na kwamba kwa kuwaleta pamoja wadau wa fani hizo kupitia blog hiyo ni suala la heshima.
Rwechungura alisema Watanzania wengi wamekuwa wakikosa blog zenye mlengo wa fani zao wazipendazo na kwamba blog hii itasaidia pia kutengeneza mawazo chanya ya Watanzania.
"Hii blog pia itachochea maendeleo ya Watanzania kwa maana ya ubinifu na uanzishaji wa michanganuo mbalimbali ya kibiashara"
Alisema matangazo mbalimbali kibiashara pia yatapokelewa ili kuyafikisha kwa wadau mbalimbali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment