YANGA WARUDISHWA NYUMBANI NA AL-AHALY!!

Mechi ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al- Ahaly ya Misri iliyopigwa kwenye uwanja mkuu wa Taifa imeonyesha jinsi timu ya Yanga ilivyokuwa imezidiwa kimpira na kuonyesha udhaifu mkubwa katika mchezo huo ambao Yanga ililambwa goli moja 1-0 hivyo kukatisha safari yao ya kuendelea na michuano hiyo kwa kutolewa na Al- Ahaly kwa magoli 4-0. Awali timu hizo zilikutana nchini misri wiki mbili zilizopita ambapo yanga pia waliambulia kipigo cha magoli 3-0 wakati timu hizo zilipocheza jijini Cairo.
Yanga waliuanza mchezo kwa kasi kubwa kitu kilichokuwa kikileta matumaini kuwa huenda timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani ingeweza kufanya maajabu, lakini kadri dakika zilivyokuwa zikienda hasa baada ya kupokea kipigo cha goli la kwanza katika dakika ya nne tu ya mchezo lililofungwa na mchezaji wa kulipwa Muangola Flavio, Yanga waliendelea kupunguza kasi yao hivyo kuwapa nafasi Al- Ahaly kutawala karibu kipindi chote cha mchezo huo.

Al Ahaly wamedhihirisha kuwa ni timu bora barani Afrika na Dunia kwa ujumla kutokana na kiwango walichokionyesha leo katika mchezo huo lakini pia rekodi yao imekuwa ya mafanikio kwa muda mrefu sasa ambapo wameshachukua kombe hili karibu mara mbili na bado wameshashiriki mara mbili katika michuano ya klabu bingwa za dunia michuano ambayo kwa sasa Manchester United ya Uingereza inashikilia kombe hilo ililolichukua nchini Japan mwaka jana haya jamani wana Yanga karibuni katika mechi zetu za ndondo tuendeleze libeneke la mpira wetu wa kibongobongo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment