Kamati inayoaandaa tuzo za Kilimanjaro Music Award 2009 leo imetangaza wanamuziki watakaopamba usiku huo wa kutoa tuzo za Kilimanjaro zinazofanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho jumamosi.
Akizungumza na wanahabari katika ukumbi huo mmoja wa waratibu wa shughuli hiyo ambaye pia ni meneja wa kinywaji cha Kilimbanjaro Lager Oscar Shelukindo amewataja wanamuziki hao kuwa ni Nemles kutoka Kenya, Blue 3 kutoka Uganda, na kutoka Tanzania ni Wanne Star, Twanga Pepeta, TID, AY, Keysha, Makamua na QJ.
amesema Tuzo za mwaka huu zimegawanyika katika vikundi 20 ambapo wasanii wa miondoko mbalimbali watashindania tuzo hizo wasanii, waliopo kwenye vikundi walichaguliwa na umma wakati wa uteuzi wa kwanza kupitia ujumbe mfupi uliokuwa ukitumwa katika simu , barua pepe na barua za posta.
0 comments:
Post a Comment