UBALOZI WA RWANDA NCHINI WAWAKUMBUKA WALIOKUFA KATIKA MAUAJI YA KIMBARI MWAKA 1994!!

Huu ulikuwa ndiyo ujumbe katika mabango kwa watu waliohudhuria maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini leo jioni pata matukiao mbalimbali katika picha chini.

Balozi wa Rwanda nchini Mh. Zeno Mutimura akisoma hotuba wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya watu waliokufa katika maauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 miaka 15 iliyopita mauaji hayo yamebaki kumbukukmbu muhimu kwa Taifa la Rwanda na nchi jirani na imekuwa ni funzo waafrika ili kutorudia makosa kama hayo tena katika nchi zetu za kiafrika.

Katibu mkuu wa Wizara ya mbambo ya nje Balozi Francis Malambugi aliyekuwa mgeni rasmi akisoma hotuba katika maadhimisho hayo.


Sekretari wa Ubalozi wa Rwanda nchini Christin Bagumo kulia na katibu mkuu wa ubaliozi huo Amutonyi Shakila wakibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo katika ukumbi wa Karimjee jijini.

Mwanamuziki Chid Benz na Afisa Uhusiano wa UN nchini Usia Nkhoma Ledama waliteta kidogo yaelekea mwanamuziki huyo anahitaji udhamini zaidi katika kazi zake za kimuziki.

Mwanamuziki Nakaaya Sumari akichangisha fedha kwa ajili ya kusaidia yatima waliotokana na mauaji hayo zaidi ya shiligi 600000 zimepatikana katika harambee hiyo na uchangiaji unaendelea kwa mtu yeyote atakayejisikia kuchangia.

Mwakilishi wa umoja wa Matifa UN nchini Oscar Fernandez akisoma ujumbe uliotolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon juu ya maadhimisho ya nchi ya Rwanda na umoja huo kukumbuka marehemu waliokufa katika mauaji ya kimbari wakati wa machafuko ya mwaka 1994.

Mwanamuziki Nakaaya Sumari wa tatu kutoka kushoto akiongoza wenzake katika kuimba wimbo I am an Afrika unahamasisha waafrika kuwa kitu kimoja katika kupambana na machafuko kama yaliyotokea nchini Rwanda Miaka 15 iliyopita katika maadhimisho ya kuwakumbuka waliokufa katika machafuko hayo Nakaaya alishirikiana na wanamuziki Sauda Simba, Chid Benz, Enika, Lufunyo na bendi ya Zemkala .

Mwakilishi wa umoja wa mataifa nchini UN Oscar Frnandes Taranco kulia, Balozi wa Rwanda Zeno Mutimura na Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje Balozi Francis Malambugi wakiwasha mishumaa kama ishara ya kuwakumbuka marehemu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda katika ukumbi wa Karimjee jioni leo.

Wanamuziki Lifunyo , Chid Benz, Nakaaya na Enika wakiwasha mishumaa kama ishara ya kuwakumbuka watu waliokufa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda miaka 15 iliyopita kumbukumbu hiyo imefanyika leo jioni katika ukumbi wa karimjee.
Afasa habari wa umoja wa mataifa UN nchini Usia Nkhoma Ledama akisoma risala wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuwakumbuka maerehemu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda leo.

wageni mbalimbali wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu waliokuokufa katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994 kumbukumbu hiyo imefanyika jioni hii kwenye ukumbi wa Karimjee jijini na kuhudhuriwa na mabalozi na wageni mbalimbalali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

5 comments:

  1. Coverage bomba ya mambo muhimu kama haya ...keep up the good work Bukuku

  2. Safi sana... artists wote should set examples like this. Vijana need rolemodels! Love the pic of the candles

  3. aise muwe mnauliza majina ya watu kabla ya kuandika - watu wengine huwa hawafurahii majina yao yakikosewa. Huyo mwakilishi wa UN ulizia jina lake - yeye ni alitumwa tu. Hilo sio jina lake umeweka kwenye picha ambayo siyo.

  4. Namuunga mkono mdau . Confirm Majina ya watu kabla ya kuandika . Wengine wameshaolewa na hawatumii majina uliyoandika. Naomba ubadilishe yawe proper - wa contct na andika upya

  5. Afasa habari wa umoja wa mataifa UN naitwa Usia Nkhoma-Ledama sio Usia Nkhoma . Cheki hata kwenye business card yake

Post a Comment