REDDS YAMWAGA MAPESA MISS TEMEKE, KINONDONI NA ILALA!!

Kulia Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel na David Minja mweneja masoko TBL na kushoto ni Jackson Kalikumtima mwandaaji wa Miss Ilala wakifunua kitambaa maalum kuonyesha uzinduzi wa udhamini mkuu wa TBL katika kanda kuu tatu za Ilala, Temeke, na Kinondoni kupitia bia yake ya Redds, uzinduzi huo umefanyika jana kwenye Club ya usiku ya Much More iliyopo Billicanas kwa matukio zaidi katika picha shuka chini mdau ujue kilichojiri katika uzinduzi huo.
Hapa wakipongezana mara baada ya uzinduzi rasmi.

Mwandaaji wa Miss Ilala Jakson Kalikumtima akiongea kutoa neno la shukurani kwa TBL jinsi ilivyoyapiga jeki mashindano hayo mkoa wa Dar es alaam kabla ya uzinduzi rasmi kufanyika kwenye Club ya usiku ya Much More pale Billicanas jana wanaofuatia ni Boy George mwandaaji wa Kinondoni Mwenyekiti wa kamati Miss Tanzania Prashant Patel Sylivia miss Tanzania namba mbili 2008 meneja masoko TBL David Minja na Mwandaaji wa Temeke Benny Kisaka.

Meneja Masoko wa TBL David Minja akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa udhamini mkuu wa kanda tatu za Miss Tanzania mkoa wa ambazo ni Temeke, Ilala na Kinondoni Kinywaji cha Redds niyo atakuwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo mkoa wa Dar es alaam.

wakubwa wakikutana haliharibiki jambo hapa Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kushoto akizungumza na Meneja masoko wa TBL David Minja wengine ni Mdau mkubwa wa Miss Tanzania Deo Kapiteni kulia, Juma pinto kati Mkurugenzi wa Jambo Concepts(Tz) Limited na mfanyabiashara kutoka Uingereza Leo Nyanduga.

Kamanda mshika Camera wa FULLSHANGWE kati akiwa katika picha ya pamoja na Ridhiwan Kikwete na Mmoja wa Maafisa wa kamati ya Miss Temeke Loveness Sekulu, jamani eti na yeye kamanda siku mojamoja akionekana kuna ubaya au mnasemaje wadau.

mwandaaji wa Miss Ilala Jackson Kalikumtima akiongea na Ridhiwan Kikwete katika hafla hiyo iliyofanyika jana Pale Much More Billicanas ni kama anasema "Bwana Mdogo hebu nipigiepigie debe basi na mimi nipate hata ukamanda wa Vijana" kushoto ni Ismail Paka rais wa timu ya Villa Squard na wengine nyuma ni kuanzia kulia ni Prashant Patel mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Benny Kisaka mwandaaji wa Temeke na Boy George mwandaaji wa Kinondoni.

Mwanamitindo maarufu Fiderin Ilanga kushoto akiwa na mwandaaji wa Miss vyuo vikuu Manka Mushi.

Jokate akipozi kwa picha na Leyla Bhanji mmoja wa waandaji wa mashindano ya urembo jijini Dar.

"Haah Jamani" Jokate Mwegelo huyo kushoto sijui anashangaa nini huku Miriam Odemba akiwa pembeni akionekana kama vile anafikiria kitu na yeye yote burudani.

Mwanamuziki Mwasiti akionyesha uwezo wake huy pia amejinyakulia tuzo ya Kili Music Award hivi karibuni.

Baba Paroko akifanya mambo kivyakevyake hii ni nzuri jamani usingoje kupewa shangwe jipe mwenyewe.

Baada ya uzinduzi kufanyika ilikuwa ni kujipa shangwe tu.

Nao Akudo Impact wakiongozwa na rapa Canal Top kushoto wakafanya mambo katika usiku wa Serengeti Lager uanaofanyika kila Jumatano pale Billicanas kamanda wa FULLSHANGWE akaona si vyema akaondoka bila kuwaona vijana wa Masauti baada ya kutoka pale Much More.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment