NCHI KUMI KUSHIRIKI MISS EAST AFRICA 2009!!

Warembo wa East Africa 2008 wakihojiwa na wanahabari mwaka jana nchini Burundi.
Shindano la Miss East Africa mwaka huu 2009 linaloandaliwa na kampuni ya Lena
Event amesema shindano hilo linatarajiwa kushirikisha nchi nyingi zaidi baada ya nchi mbili kuongezeka zaidi ya zile nane zilizoshiriki mwaka jana,
Akizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE mkurugezi wa Lena Event na mwandaaji wa shindano hilo Lena Calist amezitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, Rwanda, Somalia, Etiopia Eritrea, D, Jibouti na Mauritius, amesema nchi nyingine ni Seyshelles Re Union na Madagascar.
Lena amesema kwamba maandalizi yanaendelea vyema ambapo mwaka huu pia shindano hilo litafanyika nchini Burundi kwa mara ya pili mfurulizo kama ilivyokuwa mwaka jana na wenyeji wetu wametuomba tuendelee kufanyia shindano hilo nchini humo tena mwaka huu kutokana na mafanikio yalipatikana mwaka jana kwa ubora wake
Asilimia kadhaa ya fedha ambayo imekuwa ikipatikana kutokana na shindano hilo inapelekwa katika moja ya nchi husika za shindano hilo kwa ajili ya kusaidia watoto yatima ambapo mwaka jana watoto yatima wa Burundi walisaidiwa, Lena amemalizia kwa kusema kesho anatarajia kutoa taarifa kamili kwa vyombo vya habari juu ya maendeleo ya maandalizi ya shindano hilo.
Hapa warembo walioshinda miss East Africa mwaka jana wakischeza ngoma ya asili ya Burundi wakati wakikaribishwa katika ikulu ya Piere Nkurunzinza hii ilikwa ni mwaka jana

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment