MWANAMUZIKI DE PLAIZIR ALA PASAKA NA WATOTO YATIMA WA (TMH) LEO!!

Kutoka kulia ni Willem kutoka Uholanzi rafiki yake na mwanamuziki Fid Q, De Plaizir, Fid Q, mtangazaji wa radio Clouds Sofia Kessy na Chid Benz wakipata chakula na watoto katika kituo cha kulelea watoto cha Tanzania Mitindo House Mwanamuziki De Plaizir amesema hata yeye alifiwa na wazazi wake wote wawili miaka mingi iliyopita hivyo alilelewa na wasamaria wema tu, hivyo akaahidi kuwa yeye kama mwanamuziki hana uwezo mkubwa isipokuwa anaweza kusaidia kwa kukusanya michango kwa watu mbalimbali nchini Uingereza mara atakaporudi huko na chochote kitakachopatikana atakiwakilisha kituoni hapo ili kisaidie watoto hao ambao wanahitaji lishe nzuri na madawa kutokana na matatizo yao kwa picha zaidi za tukio hili shuka chini mdau ili upate kujua yaliyojiri katika kituo hicho
Jamani Kiongozi wetu (Mperi Nsekela) alionyesha utu wema kama unavyomuona katika picha akiungana na watoto yatima hawa wa Tanzania Mitindo House kupata pilau la pasaka pamoja na De Plaizir huu ndiyo upendo jamani wadau.

Mtoto Mariam anayelelewa kituoni hapo akimlisha keki mwanamuziki De Plaizir kama ishara ya kumkaribisha kituoni hapo kwa chakula cha mchana leo mwanamuziki De Plaizir ni mkongo anayefanya kazi zake za muziki nchini Uingereza.

De Plaizir akikata keki kwa pamoja na watoto wa TMH wakati alipokwenda kula chakula cha mchana na watoto hao katika kusherehekea sikukuu ya pasaka leo mchana nyuma kushoto ni mkuu wa kituo hicho Khadija Mwanamboka.

De Plaizir katikati na Khadija Mwanamboka ambaye ndiyo mkuu wa kituo hicho wakipiga picha ya pamoja na watoto mara baada ya mwanamuziki huyo kutoka Uingrerza kuwasili kituoni hapo leo kulia nyuma ni mtangazaji wa Radio Clouds Sofia Kessy.

Kulia mbunifu wa mavazi Franco na Fidelin pamaoja na marafiki zao wakijadili jambo wakati wakisubiri ugeni huo leo katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House.


Khadija Mwanamboka katikati Fidelin Ilanga na mmoja wa wahusika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House wakiwa tayari kupokea wageni wakati mawanamuziki De Plaizir alipotembelea kituo hicho na kula pasaka pamoja na watoto hao leo mchana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment