Kiongozi na mimbaji wa Jahazi Molden Taarab Mzee Yusuf akijimwaga na mmoja wa mashabiki wake wakati wa onyesho la bendi hiyo maalum kwa ajili ya pasaka liliofanyika kwenye Hoteli ya Travertine Magomeni usiku wa kuamkia leo ambako kulikuwa kumefurika watu kiasi kwamba hata jinsi ya kupita ilikuwa ni ngumu kweli, Mzee Yusuf na Jahazi yake amedhihirisha kuwa ni mwamba katika muziki wa taarab kwa sasa kwani ni juzi tu ambapo amejipatia tuzo mbili za Kilimanjaro Music Award zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, mdau kwa matukio zaidi hebu shuka chini upate kujua kilichojiri katika onyesho hilo.
Usiombe uende kwenye muziki lolote utakaloambiwa ufanye utafanya tu hata kama ungeambiwa kitu usichokitaka hebu wacheki hawa mdau.
Huyu jamaa alionekana akijimwaga huku akiwa amevaa kofia ya ajabu inaelekea yeye ndiyo alikuwa amevaa kwa vituko zaidi ukumbini humo.
Mzee Yusuf akifanya mambo makubwa mbele ya mashabiki wake kwenye onyesho lao lililofanyika kwenye Hoteli ya Traveltine.
Waimbaji wa kundi la Jahazi Molden Taarab wakilisogeza jahazi la pasaka kwenye onyesho lao lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Traveltine Magomeni
0 comments:
Post a Comment