JB Mpiana na kundi zima la Wenge BCBG bado ni mwanamuziki anayetisha na mbishi sana kwenye Gemu kwa wanamuziki wanaotoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Afrika kwa ujumla mwanamuziki huyu amekuwa hashuki wala hapandi sana katika kiwango chake cha muziki lakini ukitaka kumtambua kama ni mwanamuziki mkali, ni kupitia katika maonyesho yake ambayo amekuwa akifanya katika nchi mbalimbali Duniani mwanamuziki huyu mwaka jana mwishoni mwa mwezi wa Desember alidhihirisha ukali wake wakati alipokuwa nchini Marekani katika jiji la New York ambako alifanya onyesho la kukata na shoka kwenye ukumbi wa The Fillmore kwa kwa mwaliko wa kusherehekea ushindi wa Rais Barrack Obama, ni kazi ngumu kwa wanamuziki wetu wa hapa nyumbani kufikia mafanikio haya kwani wanahitajika kuwa wabunifu sana na wenye kujifunza mambo mbalimbali ili uwe mwanamuziki wa kimataifa unatakiwa kufanya nini, ili waweze kushindana katika soko muziki wa kiamtaifa kama walivyo wenzao kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ambao wamepiga hatua kwa kiwango cha hali ya juu picha hizi mdau ni kwa hisani ya mtandao wa www.Afropop.gov. hebu shuka chini uangalie mambo makubwa ya JB Mpiana
JB MPIANA BADO ANATISHA KWENYE GEMU!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment