DECI WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWAPA USHAURI WA BURE!!

Mkurugenzi wa ufundi wa DECI Bw. Kipilimba akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo leo kuishukuru serikali na Benki kuu ya Tanzania kwa ushauri waliowapa juu ya uendeshaji wa chombo hicho ambacho siku za hivi karibuni kimekuwa kikielezwa kuwa kinafanya kazi za kifedha isivyo halali Amesema wanaomba kupewa nafasi ili waweze kujieleza ni jinsi gani wanavyofanya kazi zao, na jinsi washiriki wa shirika hilo wanavyoweza kupanda mbegu na kuvuna, ameeleza kuwa baada ya tangazo la Serikali na Benki kuu wamepata matatizo mengi kibiashara ikiwa ni pamoja na washiriki kung'oa mbegu walizopanda, lakini pia kiongozi huyo amesema juzi alitekwa na watu wasiojulikana hata hivyo mungu alimnusuru baada ya kuwarubuni watu hao na kutoroka mikononi mwao, katika picha kati ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya DECI Jackson Sifaeli na mwisho ni mooja wa wakurungenzi Bw.Timoth Oleloiting'ye

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment