Vijana wa Jangwani timu ya Yanga wamerejea leo wakitokea nchini Misri walikokwenda kukwaana na timu ya Al Ahaly ya huko katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo iliambulia kipigo cha magoli matatu kwa mtungi.
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa mwalimu J. K. Nyerere mara baada ya kurejea leo asubuhi mwenyekiti wa klabu hiyo Imani Mahugila Madega amesema ni kweli kuwa wamefungwa lakini wamerudi nyumbani kazi iliyopo ni kujipanga na kufanya mazoezi yatakayoifanya timu hiyo kufanya marekebisho ili kulipiza kisasi katika mechi yao ya marudiano itakayopigwa hapa nyumbani wiki tatu zijazo yanga inahitaji kuifunga Al Ahaly magoli 4-0 ili iweze kusonga mbele katika michuano hii FULLSHANGWE tunawatakia mafaniko wanayanga wote ili muweze kushinda mtihani huu na kusonga mbele.
0 comments:
Post a Comment