Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Efraim Mafuru kushoto akipeana mkono na Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga katika picha iliyopigwa kwenye uzinduzi wa mwaka jana, Vodacom imekuwa ikidhamini mashindano hayo kwa muda mrefu sasa.
Mashindano ya Miss Tanzania 2009 yanatarajiwa kuzinduliwa kesho jumatano tarehe 18 machi katika Hotel ya Regency Park iliyoko Msasani jijini Dar katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga imesema shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa 12.00 jioni
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mara bada ya uzinduzi kutafuatiwa na semina ya mawakala wote ngazi ya mikoa na kanda yanayoandaliwa na kampuni ya LINO INTERNATIONAL AGENCY LTD, ambyo itafanyika siku mbili kuanzia tarehe 19- 20 katika Hoteli hiyohiyo ya Regency Park kuanzia saa tano asubuh, haya wadau mambo ndo hayoo yameanza hebu tuone mwaka huu tutapanda nini na tutavuna nini.
1 comments:
uzuri ni kwamba tz tunajitahi sana kuandaa matamasha ya michezo ila kila mtu anataka kula kwa kuumia mkono wake.watu wanaigia kwa kiingilo kikubwa pesa mnapeleka wapi?ubu angalia tamasha la miss tz mtafikiria ukumbi wa chang,aa manzese samahani kwa kuwaingilia ila tu nawakumbusha.
Post a Comment