WANAWAKE WAADHIMISHA SIKU YAO KWA KUONYESHA KAZI ZAO!!

Wageni kutoka Norway Anne kushoto na Graziella Van Den Bergh wa chuo kikuu cha Bergen University College wakijinunulia vitu mbalimbali wakati walipotembelea maonysho ya akina mama yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Akina mama Idaya Salum, Violet Mkwawa na Mariam Abdu wanaofadhiliwa na shirika la Care International wakiuza vikapu maalum vya kuwekea maua vilivyotengenezwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia majani makavu katika maonyesho ya wakina mama wajasiriamali katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja leo.

Lilian Sadik kutoka Care International akitoa ushauri na kugawa kondomu kwa watu waliotembelea maonyesho hayo katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwenye maonyesho ya akina mama wajasiriamali wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini mgeni wa heshima akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es alaam Abas Kandoro.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Blog yako nzuri!Nimevipenda vikapu hivi,hawa akina mama wauza vikapu wanapatikana wapi kama mtu anataka kununua vikapu.Asante na kazi njema.

Post a Comment