WALEMAVU WAANZISHA BENDI, ITAITWA (TUNAWEZA BAND)

Akina dada hawa ni miongoni mwa wanamuziki wa Tunaweza Band kulia Rehema Haji Mhasibu wa bendi na kushoto ni Rebeca Mwabujule mwanamuziki wakiwapiga tafu kaka zao katika mkutano na waandishi wa Habari.
Meneja wa bendi ya Tunaweza Iddi Tembo maarufu kama Pajero Panki akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo wakati akitangaza uanzishwaji wa bendi hiyo inayojumuisha wanamuziki walemavu kumi itapiga muziki wa kiutamaduni zaidi, katika picha anayefuatia ni Emanuel Mpesa kiongozi na mwisho ni Salehe Abdalla Super Mgumu, bendi yao imesajiliwa na basata kwa namba BST 3705 namba ya akaunti yao ni NMB2052307288, wazo la kuanzishwa kwa bendi hii lilianzishwa na mdau wa muziki anayeitwa Masoud Wanani wa kampuni ya CDS wadau saidieni kukuza bendi hii maana hawa waamuziki wameomba jembe wakalime hivyo tuwasaidie


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment