MR PAUL BADO YUPOYUPO KWENYE GEMU!!

Mr. Paul akiwa na rafiki yake katika picha.

Mwanamuziki mahiri wa mtindo wa Zouk Mr Paul aliyeko nchini Austrlia atakuwa mingoni mwa wanamuziki wahamiaji wanaoishi nchini humo ambao kwa pamoja watatengeneza Albamu ambayo itapatikana sokoni mwaka huu.
Akiongea nami Mr Paul amesema kuwa Kwa sasa anaingia studio kumalizia ngwe yake na Albamu hii inatengenezwa na kampuni inayoitwa Multicultural art ambapo yeye ataingiza nyimbo mbili zinazojulikana kama NATAMANI na ASANTE SANA. Nilimuuliza Mr Paul je nyimbo hizi ameongelea nini naye akanijibu “Nitarecord nyimbo mbili nyimbo zitapatikana World wide through eMusic, Amazon MP3 amd Nokia Music store worldwide, Si unajua music wa Zouk ni wa mapenzi, nyimbo hizo nazo zinamguso wa kimapenzi zaidi,
Pia Mr Paul aliongeza “Hii CD itatoka katikati ya mwaka huu. nadhani utakuwa ndio mwanzo wa safari yangu ya kimuziki hapa ughaibuni kwani tayari wanamuziki wengine wameanza kuonyesha interest ya kujiunga nproceeding.ami kuanzisha band. nitaendele kukupa info as things are habari kwa hisani ya http://spotistarehe.wordpress.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment