Lililokuwa kundi la Nchinga Sound likiongozwa na mpiga sollo maarufu nchini Adolph Mbinga linatarajia kusherehekea usiku maalum utakaoitwa (USIKU WA NCHINGA) unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Vatcan City Sinza jijini Dar.
Akiongea katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo mratibu wa onyesho hilo Bw. Nzowa amesema kwa sasa wako katika maandalizi makubwa kwa ajili ya onyesho hilo litakalojumuisha waliokuwa wanamuziki wa bendi ya Nchinga wakiwemo akina Rogarti Hega Deo Mwanambilimbi Muumin Mwinjuma na wengine wengi .
Ameongeza kuwa onyesho hilo litakalofanyika tarehe 28 mwezi machi mwaka huu litakuwa maalum kwa ajili ya kumpa pole mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Mudhihir M. Mudhihir ambaye alipata ajali na kupoteza mkono wake mmoja kwa ajali wakati akiwa katika shughuli za kijamii katika jimbo lake.
Amesema katika kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee umetungwa wimbo Mhsusi unaoitwa POLE MUDHIHIR ambao utaimbwa siku hiyo katika kumpa pole mheshimiwa huyo ambaye pia alikuwa mlezi wa bendi ya Nchinga, pia imeandaliwa zawadi itakayokabidhiwa siku hiyo kwa Mh. Mudhihir katika kutambua mchango wake kwa sanaa ya nchi yetu, katika onyesho hilo kiingilio kitakuwa ni sh 6000 na Bendi ya Kalunde ndiyo itakayosindikiza onyesho hilo.
0 comments:
Post a Comment