Na Anna Nkinda - Maelezo
17/03/2009 Musoma Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) amewataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao bali wawasaidie kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatawasaidia kujikwamua kimaisha.
Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili ya uwekezaji na ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji uliopo mjini Musoma.
“Nilikuwa nasikia kuwa eti wanawake wa mkoa huu wakipigwa na wanaume zao ndiyo wanaonekana kuwa wanapendwa sasa sijui kama ni kweli au lakini kwa kuwa leo niko na nyinyi wenyeji wa Mara nitajua kama ni kweli au la”, alisema.
Mwenyekiti huyo pia aliwataka wakazi hao kuachana na imani za kishirikina za kuamini kuwa ukiwaua walemavu wa ngozi (albino) utapata utajiri na kuwataka kuwafichua wauaji wa albino.
Mama kikwete alisema, “Kila mtu ana haki ya kuishi kama mwingine si vyema kuwafanya albino hawana haki ya kuishi na kuwaua pasipo sababu”.
“Acheni kuua albino kwani utajiri hauji kwa kuuza viungo vyao bali kwa kufanya kazi kwa bidii na kijituma kwa kufanya hivyo mtafanikiwa na kuondokana na umaskini”.
Akitoa salamu za shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzo Gaudensia Kabaka alisema kuwa semina hiyo imekuja kwa wakati muafaka kwani mkoa huo una raslimali nyingi likiwemo ziwa Victoria, mbuga za wanyama, uoto wa asili na jiografia nzuri hali inayoweza kuwavutia wawekezaji wengi zaidi.
Aliendelea kusema kuwa mara nyingi wanapozungumzia uwekezaji wanawazungumzia kina baba kwani ndiyo wanaotoka nje, ndiyo wenye mali lakini katika mkoa huo ni tofauti kwani kina mama ndiyo wanaotoka nje na kwenda kutafuta mali ikiwa ni pamoja na kuchunga.
Kabaka alisema, “Asubuhi mwanamke anaondoka nyumbani kwenda kuchunga akiwa mjamzito na anajifungua hukohuko malishoni lakini akirudi nyumbani baba anachouliza ni ngombe wangapi wamezaa kwa siku hiyo lakini si kuuliza kama mkewe amejifungua au la”.

0 comments:
Post a Comment