MUSWAADA WA SHERIA YA UTALII NA WANYAMAPORI AFRIKA MASHARIKI WAJADILIWA NA WADAU!!

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Rwanda Bi. Patricia Hajabakiga akifafanua jambo wakati wa warsha ya kukusanya maoni ya muswaada mpya wa sheria ya Utalii na Wanyamapori uliowasilishwa na mbunge Safina Kwekwe kutoka kenya ili ujadiliwe na wadau wa nchi zote washiriki wa jumuiya hiyo kabla ya kuupitishwa na bunge hilo na wakuu wa nchi husika na kuwa sheria kamili itakayosimamia masuala ya Utalii na wanyamapori kwa pamoja katika nchi zote za jumuiya ya Afrika Mashariki katikati ni mwenyekiti wa warsha hiyo na mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. George Nangare anayefuata pia ni Mbuge wa jumuiya hiyo kutoka Tanzania Photnatus Masha warsha hiyo imefanyika leo kwenye Hoteli ya New Afrika jijini na iliandaliwa kwa pamoja na TTB na EAC
Kutoka kushoto ni afisa uhusiano mwandamizi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Tengeneza na Meneja Masoko wa Bodi hiyo Geofrey Meena wakishiriki katika Warsha hiyo, Bodi ya Utalii nchini ni wadau wakubwa wa katika muswaada huo kwani ndiyo wasimamizi wakuu wa utalii nchini wanaotakiwa kufuatilia hatua kwa hatua katika uaandaaji wa muswaada huo

Wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari waliohudhuria katika warsha hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika wakifuatilia kwa makini wakati mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania Photunatus Masha hayupo pichani alipokuwa akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na washiriki.

Mwenyekiti wa mjadala huo wa kukusanya maoni juu ya muswaada wa sheria mpya wa utalii na wanyamapori kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. George Nangare akihojiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali baada ya kumalizika kwa mjadala huo katika hoteli ya New Afrika jijini leo.

Meneja masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw Geofrey Meena akibadilishana mawazo na mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya warsha ya kukusanya maoni kuhusu muswaada wa sheria ya Utalii na Wanyamapori uliowasilishwa katika bunge hilo na mbuge wa bunge hilo kutoka Kenya Mh. Safina Kwekwe ili kuujadilikabla haijwa sheria itakayotumiwa na nchi wanachama wa jumuiya hiyo.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment