MARCIO MAXIMO KUONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA!!

Marcio Maximo akiwa na wachezaji wa Taifa Stars katika mazoezi uwanja mkuu wa Taifa katika kujiandaa na moja ya mechi zilizopita

Rais wa TFF Rodger Tenga ametangaza kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars Marcio Maximo ataongeza mkataba wa mwaka mmoja mara baada ya mkataba wake kumalizika mwezi julai mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Millenium Makumbusho Tenga amesema TFF Imeridhishwa na kiwango cha mwalimu Marcio Maximo na kazi aliyoifanya hivyo wamemuomba aongeze mkataba wake na amekubali kuongeza kwa mwaka mmoja.


Tenga ameongeza kuwa wanatarajia kuongeza Pia makocha wengine watatu kutoka Brazili ambao kwa sasa TFF ianasubiri watume CV zao yaani wasifu wao, Tangu Maximo achukue timu ya taifa amefanikiwa kuijenga na kupandisha kiwango cha timu hiyo kimataifa

Pamoja na kwamba timu hiyo haikupata nafasi ya kwenda kushiriki katika kombe la Dunia litakalofanyika nchini Afrika kusini mwaka ujao 2010 lakini timu hiyo imefanikiwa kucheza Fainali za mataifa huru ya Afrika kwa wachezji wa ndani ambayo yalifanyika nchini Ivory Coast ambapo ilifungwa na Senegal ikaifunga Ivory Coast na kutolewa kwa mbinde na wazambia hivi karibuni

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment